Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi
Zimbabwe imehalalisha uzalishaji wa bangi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi ikiwa ndiyo nchi ya pili kufanya hivyo barani Afrika baada ya Lesotho iliyotoa leseni yake ya kwanza kwa kilimo cha mmea huo mwaka uliopita.
Serikali ilisema watu nchini Zimbabwe sasa wanaweza kutuma maombi ya kukuza bangi.
Hadi sasa, imekuwa ni haramu kupanda, kumiliki au kutumia bangi nchini Zimbabwe ambapo yeyote ambaye atakutwa na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 12 jela.
Waziri wa afya David Parirenyatwa alichapisha sheria zinazowaruhusu watu na kampuni kupewa leseni ya kufanya kilimo cha bangi ambayo hufahamika nchini humo kama mbanje.
Leseni hiyo inatakuwa inaombwa upya kila baada ya miaka mitano na itawaruhusu wakulima kumiliki, kusafirisha na kuuza bangi.
Watuma maombi watatakiwa kueleza ni wapi watafanyia kilimo chao, kiwango ambacho wataweza kuzalisha na kuuza na wakati wa kuzalisha bangi hiyo.
Post a Comment