Fahamu Ugonjwa wa Minyoo na Tiba kwa Ng'ombe - MifugoVets.


Magonjwa ya ng'ombe


Ndugu mkulima na mfugaji, leo napenda tujulishane na kukumbushana kuhusu baadhi ya magonjwa ya ng'ombe. Leo tutaangalia na kujadili aina moja ya gonjwa kati ya magonjwa mawili ambayo nimepanga kuzungumza nawe.


I. MINYOO YA NG'OMBE.

Ugonjwa wa minyoo husababisha hasara kwa mfugaji wa ng'ombe . Utafiti unaonyesha kuwa ng'ombe wengi wanaathirika na minyoo hiyo hupunguza uzalishaji. Aidha utafiti unaonyesha kuwa tatizo la minyoo kwa ng'ombe limeenea hapa nchini kwetu.

 AINA ZA MINYOO.


  • Minyoo inayoathiri ng'ombe imegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo;
  • Minyoo inayoishia kwenye maini ya ng'ombe (liverflukes).
  • Minyoo inayoishia kwenye mapafu (lungworms).
  • Minyoo mikubwa ya mviringo (large roundworms).
  • Minyoo midogo ya mviringo (small roundworms).



Dalili za ng'ombe mwenye ugonjwa wa minyoo.


  • - Kupoteza uzito
  • - Kukosa hamu ya kula
  • - Kuhara
  • - Kupungukiwa na damu
  • - Kuwa na homa
  • - Afya yake kufifia na hatimaye kufa
  • - Tumbo kuwa kubwa kupita kiasi (ndama).



Namna ya kutibu.
Wanyama wapewe dawa za kutibu minyoo mara kwa mara.

Mfano:

  1. NILZAN
  2. NILVERM
  3. PIPERAZINE
  4. ANACUR
  5. THIABENDAZOLE
  6. YOMESAN
  7. OXYDOZIDENE



Madhara ya minyoo.

  1. Husababisha upungufu wa damu.
  2. Husababisha upungufu wa maziwa.
  3. Ng'ombe huweza kufa.


Unataka kujua ni magonjwa gani mengi ambayo huathiri ng'ombe kwa kiwango kikubwa? Usikose kusoma hapa tena siku ya kesho.

2/Post a Comment/Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post

Download App

Sidebar Ads

Download App

Sidebar Ads