Jifunze Kutibu Ndui kwa Shubiri (Aloe Vera) - MifugoVets.

Dawa Tiba Kutokana na Shubiri Mwitu (Aloe Vera).
Dawa ya vidonda vinavyotokana na Ndui ya kuku au vidonda vingine vyovyote:

Dalili ya Ndui;
_ Kuku hupata vipele vya mviringo kwenye upanga wake wa kichwani, kwenye masikio,miguuni na kwingineko kusikokuwa na manyoya.

Kuandaa;
- Chukua majani ya Shubiri mwitu na kuyachana vipande vidogo vidogo. Vitwange na
pumba kidogo na kuvianika.
- Vikiisha kauka vitwange na kuchekecha upate unga laini.
- Hifadhi unga katika chombo kisafi na kikavu.

Kutumia;
- Safisha vidonda vilivyotokana na ndui au vidonda vyovyote vile na maji ya vugu vugu safi yaliyo na chumvi kiasi.
- Pakaa unga wa Shubiri mwitu katika vidonda vilivyosafishwa.
- Rudia baada ya siku moja. Tumia hivyo hadi vidonda vikauke.

NAMNA YA PILI YA KUANDAA DAWA HII;
Shubiri mwitu  ukikata jani lake huwa linatoka utovu/maji maji ( angalia picha)
Baada ya kusafisha vidonda vya ndui na maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi na wakati huo unavisafisha hakikisha unavibandua.

Utachukua jani la shubiri mwitu na kulikata yale maji maji yatakayotoka utayadondoshea kwenye vidonda vya ndui.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Download App

Sidebar Ads

Download App

Sidebar Ads