Njia Bora ya Kuzingatia katika Ulishaji Kuku - MifugoVets.

MAMBO MUHIMU KATIKA ULISHAJI KUKU.
Zingatia haya:

1.   MAJI
Maji ni muhimu sana kwa kuku wawapo bandani.
Wape maji ya kutosha kila wakati unapoona yanapungua ili waendelee kuyeyusha chakula wanachokula na kupunguza joto mwilini.
Kuku 1 anaweza kunywa hadi robo lita ya maji kwa siku.
Kwa hiyo utawawekea kulingana na wingi wao. Pata chombo kizuri ili uwaning’inizie juu kidogo kutoka usawa wa ardhi. Hii itasaidia kupunguza kuchafuka kwa maji na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya maji. kama vile kipindupindu kwa kuku na homa nyingine za matumbo
Hakikisha kuwa maji ni safi na salama.

2.    CHAKULA.
Ni vema kutafuta vifaa vizuri kwaajili ya kuwawekea chakula.
Tafuta vyombo ambavyo utaweza kuning’iniza/tundika juu kidogo kutoka chini kulingana na umri wa kuku. Hii itasadia sana kupunguza uwezekano wa kutosambaa kwa magonjwa hasa yale yanayoenezwa kupitia viatu tunavyo vaa tunapoingia bandani.
Pia itasaidi sana kupunguza chakula kinacho mwagika chini wakati kuku wanapokula.
Chakula cha kuku ni ghari ,Hivyo ni vema kufuata taratibu vizuri katika ulishaji na kutengeneza/kununua vyombo ambavyo kuku hataweza kumwaga chakula.
Kumbuka kwamba kama vyombo siyo vizuri basi vitamwaga chakula kingi na hivyo kukuletea hasara.

Ili kuweza kupata mazao mazuri yenye faida, ni vema ununue chakula cha kuku madukani au utengeneze wewe mwenyewe kama nilivyoeleza hapa chini ili uwape kuku wako chakula chenye viini lishe vyote muhimu kwa kuzingatia umri wa kuku ulionao.
Kwa vifaranga, unaweza kuwawekea chakula chini kwenye magazeti/mifuniko ya ndoo/sahani.
Baada ya siku 10 unaweza kuwawekea kwenye chombo maalum.
Pia tembelea website yetu kupata makala zaidi

Namna ya kuandaa chakula cha kuku.
Vyakula vya kuku vinapaswa kuwa na aina/viini lishe muhimu kama vile Protini, Wanga, madini na Vitamini.

Vyakula hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo;
-Vyakula vya kujenga mwili ni; Jamii ya kunde,samaki, dagaa,mashudu ya ufuta/alizeti/pamba,
-Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi ni; Mafuta ya samaki na majani mabichi kama vile; kabichi, mchicha,majani ya mpapai na nyasi mbichi.
-Vyakula vinavyojenga mwili/mifupa ni kama vile; Aina za madini, chokaa, chumvi na mifupa iliyosagwa.
- Vyakula vilivyotajwa vinaweza kumkuza vizuri kuku hadi uuzwaji/kuliwa kwake.
- Surghum Larrymeal huzuia kudonoana, huboresha kiini cha yai na kuongeza mayai. Changanya kg 1 kwa kg 50 za pumba.
 Ukosefu wa madini
  Phosphorus &Calcium- husababisha Matege,
Vidole kukunjamana,
Kufyatuka kwa misuli ya magoti, Kuwa kilema na
Kupofuka macho kwa kuku.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Download App

Sidebar Ads

Download App

Sidebar Ads