Jifunze Magonjwa, Dalili na Tiba/Chanjo kwa Mifugo - MifugoVets.

Mfugaji anatakiwa kuzingatia afya ya mnyama ili pato liweze kuwa la kuridhisha. Hapa Tanzania magonjwa yanayosumbua nguruwe sio mengi lakini hutokea mara kwa mara kufuatana na umri, mazingira na afya ya mnyama.

Magonjwa huleta hasara kwa mfugaji kwani huweza kusababisha vifo, kupunguza uzito, ukosefu wa damu hasa kwa watoto na nguruwe kudumaa. Kwa hiyo ni vizuri kuyazuia na kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo mara uonapo afya ya mnyama inabadilika.
Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa yanayoshambulia nguruwe hapa nchini.

1.Homa ya Nguruwe
(African Swine Fever):

Husababishwa na;
- Virusi
· Nguruwe wagonjwa kuchanganyika na wasio wagonjwa
· Kula chakula chenye virusi
· Kupe laini

Dalili za ugonjwa;
· Homa kali (41°C)
· Kuhema sana
· Kushindwa kala na kutembea
· Rangi ya ngozi hugeuka kuwa bluu au nyekundu
· Kifo baada ya siku 7.
· Kuharisha
· Huenea kwa kasi baada ya kutokea.

 Hakuna Tiba wala chanjo
· Nunua nguruwe kwenye mashamba yasiyo na historia ya ugonjwa
· Usafi wa vifaa, banda na mazingira yake
· Nunua vyakula vilivyothibitishwa
· Usitumie masalia toka sehemu zenye ogonjwa
· Tumia dawa za kuua kupe.
· Nguruwe wagonjwa wachinjwe.

2.Ugonjwa wa Ngozi:

Husababishwa na;
· Ukosefu wa vitamini
· Huenezwa na Viroboto, Chawa, Inzi na Utitiri

Dalili zake;
· Kujikuna mara kwa mara.
· Uvimbe kwenye ngozi.
· Hushindwa kula vizuri
· Hupungua uzito

Tiba/Chanjo
· Ogesha nguruwe vizuri.
· Tumia dawa ya kuua viroboto, chawa, Inzi na utitiri
· Lisha nguruwe chakula chenye vitamini na madini ya kutosha.

3.Kichomi
(Pneumonia)

Husababishwa na;
Bakteria.

Dalili za ugonjwa;
· Homakali
· Kupumua harakaharaka na kwa nguvu
· Kikohozi kikavu

Chanjo/Tiba;
· Hakuna tiba
· Kiua bakteria hutumika kuzuia nmyama kushambuliwa na magonjwa mengine.
· Kuwatenga wanyama.
· Nyumba iwe na hewa na joto la kutosha.

4.Midomo na Miguu

Husababishwa na;
Virusi

Dalili za ugonjwa;
· Huenea kwa kugusana mnyama mgonjwa na mzima au kula chakula chenye virusi
· Huwa na malengelenge miguuni, kwenye kiwele, midomoni na kooni.
· Hushindwa kula na kutembea.

Chanjo/tiba;
· Hakuna tiba
· Apewe ohanjo
· Asipewe chakula chenye virusi
· Tibu Vidonda
· Karantini ya sehemu yenye ugonjwa.

5.Kimeta
(Anthrax)

Husababishwa na;
Bakteria

Dalili za ugonjwa;
· Uvimbe kwenye mgongo
· Kupumua kwa tabu.
· Kifo cha ghafla
· Damu isiyoganda hutoka katika sehemu zilizo wazi kama mdomoni, masikioni na puani.

Chanjo/tiba;
· Apewe chanjo
· Nguruwe mgonjwa asichinjwe na aliyekufa asipasuliwe
· Mzoga uzikwe katika kina cha zaidi ya mita mbili au kuchomwa moto
· Toa taarifa kwa mtaalam wa mifugo haraka

7.Mafua
(Swine influenza)

Husababishwa na;
Virusi
· Huenea kwa haraka kutokani na mabadiliko ya hali ya hewa

Dalili za ugonjwa;
· Hudumaa
· Hukohoa
· Homa kali
· Hamu ya kula hupungua.
· Hupumua kwa taabu
· Manyoya husimama bila mpangilio.

Chanjo/tiba;
· Hakuna tiba wala chanjo
· Banda liwe bora ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
· Zingatia kanuni za ufugaji bora.

8.Ugonjwa wa kuharisha hasa kwa nguruwe wachanga
(Coccidiosis)

Husababishwa na;
Bakteria
· Huenea kwa mnyama kula chakula chenye bakteria hao.
· Uchafu wa vifaa na banda

Dalili za ugonjwa;
· Huharisha mharo wa kijivu uliochanganyika na kijani
· Hupungua uzito na kuwa dhaifu
· Usafi wavyombo na banda
· Wape dawa aina ya Koksidiostant


9.Ugonjwa wa Ndorobo
(Trypanosomiasis)


Husababishwa na;
Protozoa
· Huenezwa na mbung’o


Dalili za ugonjwa;
· Hupungua damu
· Hukonda
· Manyoya yanasimama
· Huweza kufa ghafla bila dalili za ugonjwa kujitokeza.


 Chanjo/tiba;
· Tumia madawa ya kuua mbung’o
· Mazingira yawe safi wakati wote.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Download App

Sidebar Ads

Download App

Sidebar Ads